Jeshi limesambazwa karibu na ofisi kuu ya chama cha upinzani cha Socialist Party Without Borders (PSF), kuligana na waandishi wa habari wa AFP.
Barabara zote zinazoelekea katika eneo la idara ya usalama wa taifa zimefungwa. Shambulio hilo linatokea baada ya mwanachama wa PSF kukamatwa na kushtakiwa kwa "jaribio la mauaji dhidi ya rais wa mahakama ya juu", serikali ilisema katika taarifa yake.
Ilisema hali inaonekana "imechukua mkondo wa kushangaza" na "mashambulizi ya makusudi ya washirika wa mtu huyu wakiongozwa na washiriki wa PSF" dhidi ya ofisi za usalama za serikali. "Hali sasa imedhibitiwa kabisa," serikali ilisema.
Serikali imesema wahusika wa kitendo hicho wamekamatwa huku wengine wakitafutwa na watachukuliwa hatua.