Washirika wa NATO watimiza ahadi kwa Ukraine

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius (kushoto) akimtazama Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov (katikati) akipeana mkono na Waziri wa Ulinzi wa Poland Mariusz huko Ujerumani, Aprili 21, 2023. Picha na Sebastian Gollnow / POOL / AFP.

Washirika wa NATO wamewasilisha karibu magari yote ya vita yaliyoahidiwa kwa Ukraine, ikiwa ni pamoja na zaidi ya magari 1550 ya kivita na vifaru 230.

Mwaka huu, Russia imefuta Michezo ya Jeshi la Kimataifa ya nchi hiyo. Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Russia "huenda ifuta michezo hususani kwa kuhofia kuwa tukio hilo lingeonekana kuwa lisilo na maana kubwa wakati huu wa vita."

Ijumaa asubuhi, Russia ilifanya mashambulizi ya makombora kwenye miji mbalimabli ya Ukraine, ukiwemo mji mkuu wa Kyiv.

Takriban watu watano waliuawa katika mashambulizi hayo. Mama na mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka mitatu waliuwawa huko Dnipro, jumla ya watu watatu nao waliuwawa katika mji Uman, uliopo katikati ya Ikraine na kujeruhi watu wengine wanane.

Uharibifu katika mji wa Kyiv haukubainika haraka.

Siku ya Alhamisi, Bunge la Baraza la Ulaya lilipitisha azimio la kutambua kwamba kitendo cha Russia cha kuwahamisha watoto wa Ukraine kina ushahidi wa mauaji ya kimbari.

Pia siku ya Alhamisi, waziri mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal, alisema alimwomba Papa Francis, wakati wa hadhira ya faragha, msaada wake wa kuwarudisha nchini Ukraine watoto “walioshikiliwa, kukamatwa, na kuhamishiwa Russia kinyume cha sheria.”

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Russia Vladimir Putin na kamishna wa haki za watoto wa nchi hiyo, Maria Lvova-Belova, kwa madai ya kuhusika kwao katika kuwapeleka watoto kutoka maeneo yanayokaliwa ya Ukraine kwenda Russia.