Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:23

Rais Xi na Rais Zelenskiy wazungumza kwa mara ya kwanza katika juhudi za kutatua mzozo kati ya Russia na Ukraine


Picha za Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Xi Jinping wa China
Picha za Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Xi Jinping wa China

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema alifanya “mazungumzo ya simu ya muda mrefu na yenye maana” na Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano, huku viongozi hao wawili wakikubaliana kutuma wajumbe wao mjini Beijing na Kyiv.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Zelenskyy hakutoa maelezo zaidi kuhusu mazungumzo yake na rais Xi, yakiwa mawasiliano yake ya kwanza rasmi na rais wa China tangu uvamizi wa Russia miezi 14 iliyopita.

Zelenskyy alisema “Ninaamini mazungumzo haya ya simu, vile vile uteuzi wa balozi wa Ukraine nchini China, vitaleta msukumo mkubwa kwa maendeleo ya uhusiano wa nchi zetu mbili.”

Baadaye kwenye tovuti yake, ameyataja mazungumzo hayo kuwa yenye tija na kusema yatatoa mwelekeo wa “uwezekano wa majadiliano kwa lengo la kuweka mazingira ya amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine.”

Vyombo vya habari vya serikali ya China vimeripoti kwamba Xi alitoa wito kwa Zelenskiy kwa ajili ya mazungumzo kati ya Russia na Ukraine, akionya kuwa “hakuna mshindi katika vita vya nyuklia.”

XS
SM
MD
LG