Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:12

Russia inaandikisha "wanaume halisi" kupigana katika uvamizi wake Ukraine


Rais wa Russia Vladmir Putin akisalimiana na baadhi ya wanajeshi wake
Rais wa Russia Vladmir Putin akisalimiana na baadhi ya wanajeshi wake

Matangazo ya kampeni mpya kwenye mabango, televisheni, na mitandao ya kijamii pia yanaelezea tuzo za kifedha kwa kujisajili katika jeshi la Russia, lakini hakuna uwezekano mkubwa kwamba Russia itafikia lengo lake la kuandikisha watu laki nne wa kujitolea, wizara ya Uingereza imesema

Russia inaangalia kuandikisha “wanaume halisi” kupigana katika uvamizi wake wa Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumapili katika taarifa yake ya kijasusi iliyochapishwa kwenye Twitter.

Matangazo ya kampeni mpya kwenye mabango, televisheni, na mitandao ya kijamii pia yanaelezea tuzo za kifedha kwa kujisajili katika jeshi la Russia, lakini hakuna uwezekano mkubwa kwamba Russia itafikia lengo lake la kuandikisha watu laki nne wa kujitolea, wizara ya Uingereza imesema.

Ukraine ilitangaza vikwazo vipya dhidi ya watu binafsi au taasisi za kisheria zinazounga mkono au kuwekeza katika uvamizi wa Russia. Katika hotuba yake ya video ya Jumamosi usiku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema kuwa Kyiv imeweka vikwazo kwa makampuni 322 ambayo yanatengeneza silaha na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la Russia dhidi ya Ukraine.

Vikwazo zaidi vimewekwa dhidi ya watu binafsi na mashirika ya kisheria ambayo yanasaidia kukwepa vikwazo dhidi ya Russia alisema. Jukumu ni kuondoa fursa yoyote kwa Russia kukwepa vikwazo aliongeza, na kwamba vikwazo vikali dhidi ya uchumi katika vita vya Russia, hivi karibuni utakuwa mwisho wa uchokozi.

XS
SM
MD
LG