Mohib Ullah alionekana katika miaka ya hivi karibuni kama mmoja wa watu mashuhuri zaidi anayewakilisha Warohingya 850,000 ambao wamekwama katika makambi nchini Bangladesh baada ya kukimbia ghasia nchini Myanmar mwaka 2017.
Watu wasiojulikana wakiwa na bunduki walimuua Jumatano jioni, na kusababisha serikali ya Bangladsh kupeleka mamia ya polisi zaidi katika makambi ya wakimbizi hao Alhamisi.
Takriban watu 25,000 walihudhuria sala ya mazishi yake katika kambi kuu ya Kutpalong Alhamisi, kwa mujibu wa polisi.
Lakini kiongozi mwingine wa Warohingya Nazir Hossain anasema waliohudhuria walikuwa 200,000.
Habib Ullah ameiambia AFP kwamba katika miezi ya hivi karibuni kaka yake alipata vitisho vya kuuawa kutoka kwa jeshi la uokovu la Arakan Rohingya na kwamba takriban wanaume wanane kutoka kundi hilo walihusika katika shambulizi hilo.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la AFP