Wanajeshi hao wamekutikana na makosa kwa kuhusika na mauaji ya raia wawili wa China, waliouliwa Machi 17 2020, katika wilaya ya Mambasa.
Raia hao waliouawa walikuwa na madini katika gari yao wakitokea katika migodi.
Miongoni mwa walio hukumiwa baada ya jeshi kusikilizwa keshi hizo ni makanali wawili wa jeshi ambao ni maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Congo.
Mahakama hata hivyo imemuachilia raia mmoja aliyekamatwa katika kesi hiyo kulikuwa hakuna ushahidi wowote kuwa alishiriki katika mauaji ya raia wa China walio kuwa wakichimba dhahabu mkoani Ituri.
Wakaazi katika mji wa Bunia waipongeza mahakama ya kijeshi. Mama Julie mkazi wa Bunia, anasema kafurahi kuona mahakama imechukua hatua nzuri ambayo ni onyo kwa wanajeshi wa Congo .
Mama Chritsine mke wa askari mmoja aliye hukumiwa amesema mume wake amehukumiwa bure kwani mumewe alikuwa mlinzi wa wakuu, anashangaa kuona mumewe kahukumiwa miaka kumi jela japo yeye hakuhusika katika mauaji hayo, ni vyema mahakama ya kijeshi imuachilie.
Wazee wa mkoa wa Ituri walisema mahakama imewajibika vyema kwani kuna makosa yanayo tekelezwa na wanajeshi watiifu kwa serikali lakini bila ya kuadhabiwa. Hivyo kuwahukumu hao maafisa wa ngazi ya juu ni somo kwa wenzao alisema Wakarara mzee wa Bunia.
Hukumu hiyo imejiri baada ya karibu wiki moja ya kuwasikiliza washtakiwa na Ijumaa kutolewa adhabu.
Mahakama hiyo ya kijeshi imewahukumu kwa makosa ya mauaji, kushirikiana na majambazi, wizi, n.
Imeandaliwa na mwandishi wetu Austere Malivika, Goma, DRC.