Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 16:37

Wakaazi waliokimbia  Rutshuru DRC waomba jeshi la Afrika Mashariki kuwasaidia haraka

Wakaazi wialayani Rutshuru waomba jeshi la Congo FARDC na la Afrika Mashariki kurejesha usalama kwenye vijiji vyao kwa haraka.(Malivika).
Wakaazi wialayani Rutshuru waomba jeshi la Congo FARDC na la Afrika Mashariki kurejesha usalama kwenye vijiji vyao kwa haraka.(Malivika).

Wakaazi waliokimbia  vijiji vyao miezi sita sasa tangu uasi wa M23 kuingia Rutshuru Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC wameomba serikali na jeshi la Afrika Mashariki kutatua kwa haraka mzozo wa M23 kwani wapitia madhila mabaya uhamishoni.

Byamungu Garubanda ni mkazi wa Bunagana pembeni ya mpaka wa Uganda alikimbia makazi yake akiwa na watoto miezi sita iliyopita na sasa akiwa uhamishoni katika mazingira magumu na ukosefu wa Chakula na hata matibabu huku watoto wake wakishindwa kwenda shuleni anaomba Muungano wa jeshi kutoka Afrika Mashariki na jeshi la Congo-FARDC kufanya juhudi zote kuwarejesha katika makazi yao ya Bunagana.

Baadhi ya wakimbizi hao wanasema wamechoka kwa sasa kuwa wakimbizi na kuishi uhamishoni wanapitia hali ngumu na mbaya wakiwa mbali na nyumbani kwao.

Serikali kwa upande wake imeomba wakazi wa mashariki mwa Congo kuwa watulivu kwani sasa jeshi la Afrika mashariki lipo njiani kuungana na jeshi la Congo kuwakamata waasi wote mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo lile la kundi la M23.

Wakati huo huo Shabola Bintou mbunge wa Chama Tawala UDPS akiwa Mjini Kinshasa amewaomba hata hivyo kwa vijana kujiunga na jeshi tiifu kwa serikali kupigania taifa lao.

Hata hivyo wananchi wengi wakiwa na mashaka wameomba serikali ya nchi hiyo kujitegemea kuliko kutegemea mataifa mengine kwa kutafuta amani nchini DRC.

XS
SM
MD
LG