Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 17:33

DRC: Wakimbizi wa ndani wasema changamoto zinazowakumba zimezidi


Kambi ya wakimbizi wa ndani katika eneo la Gisenyi, Mashariki mwa DRC. Picha na Austere Malivika.
Kambi ya wakimbizi wa ndani katika eneo la Gisenyi, Mashariki mwa DRC. Picha na Austere Malivika.

Wakazi waliokimbia vijiji vyao kutoka mji wa Irumu, wilaya ya Djugu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao wanaishi katika kambi za muda, wanaiomba serikali y kurejesha amani na usalama kwenye vijiji vyao kwa haraka, ili kupunguza changamoto zinazoendelea kuongezeka kila uchao.

Ndanguzi Esperence ni mama mjane akiwa na watoto wanne - wasichana watatu ni mvulana mmoja - na anasema mumewe aliuwawa siku zilizopita na watu wenye silaha ambao walivaamia makazi yao majira ya asubui na kumuua kwa mapanga akiwa shambani wilayani Nduju.

Kwa sasa mama huyo pamoja na watoto wake wanapitia hali ngumu ya maisha katika Mji wa Kasenyi ulio pembeni mwa Ziwa Albert, linalounganisha Uganda na Congo DRC.

Anaomba muungano wa Jeshi la Congo FARDC pamoja na UPDF kuhudumisha amani na usalama kwenye vijiji vyao ili siku siku moja warudi kulima mashamba yao wakisema wamechoshwa na hali ya kuombaomba katika mji huoulio umbali wa kilometa hamsini na saba kusini mashariki mwa Mji wa Bunia.

Sikiliza ripoti iliyoandaliwa na Austere Malivika:

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:58 0:00

Mashirika ya kutetea haki za wanawake nayo pia yanaomba serikali kupitia jeshi lake kuwajibika na kuwahakikishia wananchi wa Congo Amani hasa wale wa Ituri na kivu Kasakizini.

Mji wa kasenyi kwa sasa umepokea wakazi wengi wanaokimbia vijiji vyenye ukosefu wa usalama na hata wengine wakilamizika kukimbilia taifa Jirani la Uganda kutumia Boti na wakati mwengine huzama na kusababisha vifo vya watu wanapojaribu kunusuru maisha.

-Imetayrishwa na Austere Malivika voa, Goma, DRC.

--

XS
SM
MD
LG