Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 10:05

Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa auwawa DRC


Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo cha ukaguzi.
Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo cha ukaguzi.

Mwanajeshi mmoja wa Pakistan anayehudumu kama mlinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliuawawa katika shambulio la wanamgambo mashariki mwa nchi hiyo, jeshi lilisema

Kundi la wanamgambo sita walifika kambi ya operesheni ya kudumu ya Umoja wa Mataifa katika wilaya ya Minembwe, wakidhaniwa wanasalimisha silaha zao kama sehemu ya mpango wa Umoja wa Mataifa. Lakini kiongozi wa kundi hilo alianza kufyatua risasi kiholela, jeshi la Pakistan lilisema katika taarifa Jumamosi usiku.

Mwanajeshi wa Pakistani aliyekuwa mlinzi katika eneo la kusalimisha silaha alipigwa risasi kichwani, ilisema taarifa hiyo. Walinda amani wa Pakistan walijibu mara moja, ilisema, bila kutoa maelezo.

Mwanajeshi huyo aliyejeruhiwa vibaya, aliyetambuliwa tu kama Babar mwenye umri wa miaka 35, alikimbizwa katika kitengo cha matibabu cha karibu cha jeshi la Pakistani lakini alifariki baadaye.

Umoja wa Mataifa uliwataja watu wenye silaha katika shambulizi la Ijumaa kuwa washukiwa wa wapiganaji wa Twirwa-neho. Wanajeshi wa Pakistan walisema wanahusishwa na Banyamulenge, jamii ya Watutsi katika jimbo la mashariki la Kivu Kusini.

XS
SM
MD
LG