Wakuu wa majeshi kutoka Jumuiya ya Uchumi ya Africa Magharibi – ECOWAS wanakutana Ghana kujadili uwezekano muhimu wa kuingilia kati kijeshi nchini Niger kujibu mapinduzi yaliyofanyika mwezi uliopita.
Jana ECOWAS, imesema imeanza kukitayarisha kikosi chake maalumu ambacho kitarejesha utawala wa kikatiba katika jamhuri ya Niger.
Jumuiya hiyo ya kikanda imesema mkutano wa mjini Accra utakuwa ni kukamilisha mipango ya kupeleka kikosi hicho maalum.
Mazungumzo yanafuatia shambulizi la uasi ambapo jeshi la kijeshi la Niger limesema wanajeshi wake 17 waliuwawa.
Viongozi wa kijeshi walisema rais Mohamed Bazoum aliyeondolewa alishindwa kushughulikia ghasia zilizotekelezwa na makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.