Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:56

Wanajeshi waliopindua serikali ya kiraia Niger wasema watamfungulia mashtaka ya uhaini Rais Mohamed Bazoum


Wanajeshi waliofanya mapinduzi Niger
Wanajeshi waliofanya mapinduzi Niger

Utawala wa kijeshi uliokamata madaraka Niger kwa njia ya mapinduzi mwezi uliopita umesema utamfungulia mashtaka rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum kwa uhaini mkubwa kutokana na mawasiliano yake ya wakuu wa nchi za kigeni na mashirika ya kimataifa.

Viongozi wa mapinduzi wamemfunga Bazoum na kuivunja serikali iliyochaguliwa, hali iliyosababisha ukosoaji mkubwa kutoka mataifa ya kigeni yenye nguvu na nchi jirani za Afrika Magharibi ambayo yametayarisha jeshi la dharura ambalo linaweza kuingia Niger kumrejesha Bazoum.

Rais wa Niger Mohamed Bazoum
Rais wa Niger Mohamed Bazoum

Msemaji wa serikali ya kijeshi Kanali Amadou Abdramane amesema katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni Jumapili kwamba mamlaka za kijeshi zimekusanya ushahidi wa kutosha kumshitaki rais aliyepinduliwa kwa uhaini mkubwa na kupuuzia usalama wa ndani na nje wa Niger.

Kanali Amadou Abdramane mjumbe wa Baraza la Taifa la Kulinda Maslahi ya Nchi CNSP liliundwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi : “Kwa vyovyote vile, serikali ya Niger hadi sasa imekusanya ushahidi unaohitajika kumfungulia mashtaka rais aliyeondolewa madarakani na washirika wake wa ndani na nje mbele ya vyombo husika vya kitaifa na kimataifa, kwa uhaini mkubwa na kudhoofisha usalama wa ndani na nje wa Niger, kufuatia mazungumzo yake na raia wa nchi hiyo . wakuu wa nchi za kigeni na wakuu wa mashirika ya kimataifa.”

Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Marekani na Umoja wa Mataifa wote wamesema wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Bazoum.

Chama cha siasa cha Bazoum kimesema familia yake haina maji, chakula au hata madaktari na Bazoum ameliambia shirika la haki za binadamu, human rights watch kwamba mtoto wake wa kiume anahitaji kumuona daktari kutokana na hali mbaya ya moyo.

Forum

XS
SM
MD
LG