Zaidi ya watu milioni moja Chad wakiwemo wakimbizi wanakabiliwa na hatari ya kutokua na chakula na msaada wa dharura, endapo misaada haitaongezwa, limesema Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa- WFP.
Katika kambi za wakimbizi huko Mashariki mwa Chad ukosefu wa maji safi ya kunywa na huduma za msingi za hifadhi ya maji taka zinasababisha kuenea kwa magonjwa hatari.
Maafisa wa Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF wamesema wamerekodi zaidi ya watu, 1,000 wenye ugonjwa Hepatitis E umeenea katika kambi zilizoko Mashariki mwa Chad ambao tayari umesababisha wanawake wajawazito kufariki.
Mratibu wa mungano wa mashirika ya misaada kwa ajili ya kanda hiyo Mraie Jose Alexander, amesema Ijumaa kuwa katika kambi ya Metche, ambayo inahifadhi wakimbizi 40,000, watu wako katika uhitaji mkubwa wa maji, chakula, makazi na huduma msingi za kuondoa uchafu.