Warepublikan wanadai wanataka kuleta hoja ya kwamba vyombo vya usalama vya serikali kuu vinakashfa ya kuegemea upande mmoja kisiasa.
John Durham, ambaye hivi karibuni amekamilisha ripoti yake kuhusu uchunguzi wa Shirika la Upelelezi la FBI juu ya kampeni ya Trump ya 2016, atatoa ushahidi Jumatano mbele ya Kamati ya Sheria ya Baraza la Wawakilishi.
Hilo linajiri siku moja baada ya Durham kukutana kwa faragha na wajumbe wa Kamati ya Upelelezi ya Baraza la Wawakilishi.
Wakati Durham amekuwa na kesi tatu – huku mbili zikiwaachia watuhumiwa – katika uchunguzi wa miaka minne, ripoti yake imegusia wafanyakazi wa FBI kutowapa taarifa muhimu majaji na wanapinga ofisi hiyo kupuuzia sababu za kutochunguza kampeni ya Trump.
Warepublikan ambao wanadhibiti Baraza la Wawakilishi wanasema bado wamekasirishwa kuhusu uchunguzi wa kampeni ya 2016, inayojulikana kama “Crossfire Hurricane,” na wanakusudia kushinikiza vizuizi vipya kwa FBI wakitaka kutazamwa upya mamlaka ya kufanya uchunguzi inayojulikana kama Kifungu 702 ambacho vyombo vya usalama vya Marekani vinakiona ni muhimu sana na kwamba kumalizika muda wake mwisho wa mwaka huu.
Pia Wademokrat wengi wanataka kanuni mpya juu ya uwezo ambao FBI unaweza kuwa nao kuchunguza takwimu za nje juu ya taarifa kuhusu raia na makampuni ya Kimarekani.
Chuki ya Chama cha Republikan dhidi ya Wizara ya Sheria imechochewa Jumanne baada ya tangazo la kuwa mtoto wa Rais Biden, Hunter kuna uwezekano hatokwenda jela katika makubaliano yaliyofikiwa juu ya madai ya kodi na silaha.
Mwakilishi Mrepublikan Jim Jordan wa Ohio, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, alituma ujumbe wa Twitter, kwa herufi kubwa, kuwa “huo ni upendeleo wa kisheria.
Taarifa hii inatokana na shirika la habari la AP.