Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 00:12

Hunter Biden atakiri makosa mawili kwa waendesha mashtaka wa serikali kuu


Hunter Biden, mtoto wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden. April 18, 2022.
Hunter Biden, mtoto wa kiume wa Rais wa Marekani Joe Biden. April 18, 2022.

Kama sehemu ya makubaliano hayo Idara ya Sheria imekubali kupendekeza hukumu ya mashtaka kwa makosa mawili ya kushindwa kulipa kodi kwa wakati unaofaa kwa mwaka 2017 na 2018 kulingana na vyanzo

Hunter Biden, mtoto wa kiume wa Rais Joe Biden, atakiri makosa mawili ya utozaji kodi na kufikia makubaliano na waendesha mashtaka wa serikali kuu kutatua mashtaka ya uhalifu, Idara ya Sheria imesema Jumanne katika kesi iliyofunguliwa mahakamani.

Mashtaka hayo yalielezewa kwa kina katika jalada la uhalifu katika mahakama ya wilaya ya Delaware, mahala ambapo mwanasheria wa Marekani David Weiss, mteule wa Trump, amekuwa akifanya uchunguzi ambao wakati mmoja ulichunguza madai ya utakatishaji fedha, na mashtaka mengine. Profesa David Monda kutoka chuo kikuu cha New York nchini Marekani anaelezea hatua hii ina maanisha nini kwa Rais Joe Biden ikijumuisha pia utawala wake.

Mahojiano ya Profesa David Monda na Kumekucha Afrika ya VOA Swahili.m4a
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:14 0:00

Forum

XS
SM
MD
LG