Kudhibiti chuki dhidi ya Uislam, Waislam Marekani wamtaka Biden aagize kusitishwa mapigano Gaza

Mkutano wa Waislam wa Marekani kuonyesha mshikamano na Wapalestina watoa wito kusitishwa mapigano Gaza, wakati wa maandamano katika mji mkuu, Washington, Oktoba. 21, 2023.

Vikundi vya Kiislam nchini Marekani vinasema juhudi za utawala wa Biden kukabiliana na kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislam nchini Marekani lazima ziende sambamba na kuwalinda raia walioko Gaza kutokana na mashambulizi ya mabomu ya kulipiza kisasi dhidi ya Hamas.

Mashambulizi hayo yameuwa maelfu ya Wapalestina.

“Hatua ya kwanza muhimu zaidi ambayo Rais [Joe] Biden lazima achukue ni kukabiliana ongezeko la chuki dhidi ya Uislam, ni hatua ambayo viongozi wa Kiislam wa Marekani na jumuiya mbalimbali zimerejea mara kwa mara kumtaka achukue hatua:

Tunataka sitisho la mapigano huko Gaza,” Baraza hilo la America – Islamic Relations lilisema Alhamisi katika taarifa yake ikijibu tangazo la White House Jumatano kuwa uongozi wa Biden unaandaa mkakati wa kwana wa aina yake kukabiliana na chuki dhidi ya Uislam.

CAIR ni jumuiya kubwa kabisa inayotetea Waislam nchini.

Edward Ahmed Mitchell, naibu mkurugenzi wa CAIR, ameiambia VOA vita vinavyoendelea Gaza vinachochea ghasia na ubaguzi kote duniani, ikiwemo kuwalenga Wapalestina Waislam raia wa Marekani.

“Serikali yetu lazima iamuru kumalizwa kwa ghasia hizo na unyama dhidi ya Waislam na Wapalestina unaotumiwa kuhalalisha ukatili huo. Hapo tu ndipo mkakati mpana wa kuzuia chuki dhidi ya Uislam utakuwa na tija,” Mitchell alisema.

Wakati wa maelezo yake huko White House Alhamisi, John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa, alirejea uungaji mkono kwa kusitishwa kwa muda na kuruhusu juhudi kiasi za kibinadamu katika vita hivyo lakini akasisitiza sitisho la mapigano kwa sasa liwanufaisha Hamas.

Mwisho…