Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:45

Israel ya dondosha mabomu kwenye kambi ya Jabalia kwa siku ya pili mfululizo


Mtoto wa Kipalestina avutwa kutoka vifusi vya jengo lililobomolewa kwa mabomu
Mtoto wa Kipalestina avutwa kutoka vifusi vya jengo lililobomolewa kwa mabomu

Haijafahamika bado idadi ya watu walofariki au kujeruhiwa kutokana na shambulio la pili kwenye kambi hiyo ya zamani ya ukanda wa Gaza.

Israel inasema kwamba mashambulio hayo yamewauwa makamanda wawili muhimu wa Hamas na kwamba kundi hilo linaishi na kuficha silaha zake miongoni mwa makazi ya raia.

Israel inasema wanajeshi wake 16 wameuliwa katika mapambano na wapiganaji wa Hamas mnamo siku tano za mapigano ya nchi kavu.

Wapalestina wasubiri kuvuka mpaka kuingia Misri kupitia kituo cha mpakani cha Rafah
Wapalestina wasubiri kuvuka mpaka kuingia Misri kupitia kituo cha mpakani cha Rafah

Wakati huo huo karibu watu 400 wa kwanza, wageni na wapalestina waliruhusiwa kuvuka kivuko cha Rafah na kuingia Misri siku ya Jumatano.

Rais Joe Biden anasema wamarekani wa kwanza waliweza kuvuka kutokana na juhudi za kidiplomasia za serikali yake.

Kwa upande mwengine wizara ya mambo ya nje imekuwa ikiwasiliana na wamarekani ndani ya Gaza juu ya mipango yao ya kuondoka katika siku zinazokuja.

Forum

XS
SM
MD
LG