Balozi mpya wa Marekani nchini Israel aliwasili Ijumaa nchini humo kushika wadhifa wake ambao ulikuwa wazi kwa miezi kadhaa huku vita kati ya Israel na Hamas vikiendelea.
Jack Lew ambaye aliapishwa Alhamis alipanda ndege akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kuelekea Israel, mwandishi wa shirika la habari la AFP alisema.
Lew mwenye umri wa miaka 68 kutoka dhehebu la kiyahudi la Orthodox anatarajiwa kuwasilisha stakabadhi zake kwa Rais wa Israel Isaac Herzog katika siku kadhaa zijazo.
Licha ya kuwa mshirika wake wa karibu sana, Marekani haijakuwa na balozi nchini Israel tangu Julai mwaka jana. Mtangulizi wa Lew, Tom Nides aliondoka.
Wakati huo huo Blinken aliwasili Israel leo Ijumaa katika safari inayoangazia hatua za kupunguza madhara kwa raia huko Ukanda wa Gaza waliokumbwa na vita kati ya Israel na Hamas.
Hii ni ziara yake ya pili Blinken huko Mashariki ya Kati tangu kuzuka kwa vita vilivyochochewa na mashambulizi ya Hamas hapo Oktoba 7 ambapo kulingana na maafisa wa Israel watu 1,400 waliuawa wengi wao wakiwa raia.
Forum