Vyombo vya usalama vilisikia makelele ndani ya kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo katika kituo cha ukaguzi kaskazini magharibi ya jimbo la Tete, ambapo lori hilo lilisimamishwa baada ya kuvuka mpaka kutoka Malawi.
Maafisa wa usalama waligundua manusura 14 pamoja na miili ya wahamiaji wengine walipofungua mlango wa kontena hilo.
Wahanga hao wanaaminika kuwa walikufa kutokana na ukosefu wa hewa. Walionusurika walichukuliwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya eneo hilo. Dereva wa lori na mtu mwengine wamewekwa rumande.
Msumbiji ambayo iko kusini mashariki mwa Afrika ni kituo cha kupitia wakimbizi wakijaribu kuingia Afrika Kusini, moja ya nchi katika bara la Afrika yenye viwanda vingi.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.