Wachumi waonya udhibiti wa sarafu ya digitali Nigeria

Aikoni ya programu ya Binance kwenye simu mahiri, Februari 28, 2023, katika Kitongoji cha Marple, Pa. Nigeria. Picha na AP

Wachambuzi wa uchumi na wapenzi wa sarafu ya digitali wameelezea wasi wasi wao kufuatia Nigeria kupiga marufuku malipo kuanzia mwanzo mpaka mwisho — aina ya malipo — yanayohusisha sarafu ya naira, katika jukwaa kubwa zaidi duniani la soko ya sarafu ya digitali, Binance.

Kampuni ya Binance imesitisha huduma za naira siku ya Ijumaa baada ya mamlaka ya Nigeria kuishutumu kampuni hiyo kwa unyonyaji, kushusha thamani ya naira na biashara haramu ya mzungumko wa fedha.

Udhibiti wa huduma za naira kwenye soko la Binance ulifanywa siku ya Jumatatu. Lakini wakosoaji wamesema, hatua hizo zinaweza kuongeza ukosefu wa ajira kwa vijana nchini ambao tayari wanahangaika na kupanda kwa gharama za maisha.

Hatua ya hivi karibuni ya mamlaka inafuatia hatua za karibuni kujaribu kuiokoa sarafu ya Nigeria kutoporomoka na kupambana na matatizo ya kiuchumi.

Serikali pia imeishutumu kampuni hiyo kufadhili ugaidi na kufasirisha fedha, ikisema kiwango cha fedha chenye thamani ya dola milioni 26 katika jukwaa hilo hazikuweza kupatikana.

Binance imekanusha kufanya kosa lolote katika taarifa iliyoibandika katika tovuti yake mwezi uliopita.