Wanaigeria waliokata tamaa wamekuwa wakiandamana kupinga ongezeko la bei za chakula huku mzozo mkubwa wa kiuchumi ukiwalazimisha watu kuacha kula mlo mmoja na kula mchele usio na ubora unaotumika kama chakula cha samaki.
Tangu kuingia madarakani rais Bola Ahmed Tinubu ameondoa ruzuku ya mafuta na kudhibiti fedha ya nchi hiyo hali iliyopelekea ongezeko la bei ya mafuta na gharama kubwa ya maisha wakati Naira inashindana na Dola ya Marekani.
Mfumuko wa bei umeipiga Nigeria kwa miongo mitatu na kikiwa juu ya asilimia 28 mwezi Decemba , hiyo ni kwa mujibu wa idara ya takwimu ya taifa.
Hali mbaya ya maisha imechochea maandamano katika miji kadhaa ya kaskazini ikiwemo Suleja karibu na mji mkuu wa Abuja , mina katika jimbo la Niger na kitovu cha uchumi mji wa Kano.
Forum