Ethiopia: Wanahabari watatu wameuawa tangu serikali kutangaza hali ya hatari

Wahamiaji kutoka eneo la Amhara. Septemba 7, 2023.

Waandishi wa habari watatu wamekamatwa nchini Ethiopia, mwezi mmoja tangu serikali itangaze hali ya hatari mapema mwezi Agosti.

Ethiopia ilitangaza hali ya hatari ya miezi 6 hapo tarehe 4 mwezi Agosti ili kukabiliana na mzozo katika jimbo la kaskazini la Amhara.

Baraza la Wawakilishi wa nchi hiyo liliidhinisha hali ya hatari tarehe 14 mwezi Agosti, ambayo inaipatia serikali mamlaka ya kuwakamata watu bila idhini ya mahakama, kati ya nguvu zingine.

Tangu wakati huo, waandishi wa habari watatu wamekamatwa nchini Ethiopia, kulingana na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari, au CPJ. Kundi hilo la kutetea uhuru wa vyombo vya habari lilisema wanahabari wote watatu walichapisha maudhui kuhusu mzozo wa Amhara, na hali hiyo ya hatari.

Kukamatwa huko kumejiri baada ya vikosi vya usalama vya Ethiopia kuwakamata waandishi wanane mwezi Aprili, kutokana na habari walizochapisha kuhusiana na mzozoz wa Amhara na haki za binadamu, kulingana na shirika la Reporters Without Borders, RSF.

Katika taarifa Jumatano, CPJ ilikosoa kukamatwa kwa hivi punde na kuitaka serikali kuwaachilia wanahabari wote waliozuiliwa nchini humo kutokana na kazi zao.