Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:30

Mapigano ya Amhara, Ethiopia yasababisha uhaba wa chakula


Mji wa Lalibela mkoani Amhara,Ethiopia, January 25, 2022.
Mji wa Lalibela mkoani Amhara,Ethiopia, January 25, 2022.

Mivutano imeongezeka katika mkoa wa  Amhara nchini Ethiopia kutokana na mapigano ya mara kwa mara kati ya vikosi vya serikali kuu na makundi ya wanamgambo wa  mkoa huo wajulikanao kama FANO, na hivyo kusababisha uhaba wa chakula pamoja na kuathiri huduma za afya.

Shughuli kwenye miji mingi ya Amhara zimesimama kufuatia mapigano kati ya FANO na vikosi vya serikali vinavyo dhibiti miji kadhaa mikubwa. Serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya dharura kwenye mkoa wa Amhara mwanzoni mwa Agosti, na hivyo kuathiri usafiri pamoja na kugeuza makao makuu ya kiutawala kuwa kamandi ya kijeshi.

Mapigano kati ya FANO na vikosi vya serikali yalifikia kilele mwanzoni mwa Agosti baada ya miezi kadhaa ya ghasia kufuatia agizo la serikali la kuingiza wapiganaji kwa kieneo kwenye mfumo rasmi wa kiusalama wa serikali. Ripoti ya UN ya hivi karibuni imesema kwamba hali hiyo imepelekea zaidi ya vifo 180 tangu Julai.

Taarifa iliyotolewa Ijumaa na kamanda wa jeshi Field Marshall Berhanu Jula, imesema kwamba hali kwenye mkoa wa Amhara imeimarika na kwamba hakuna tena tishio la usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG