Polisi nchini Tanzania Jumatatu imewakamata viongozi wawili wa upinzani, chama chao na polisi wamesema, kwa azma ya kuzuia maandamano ya dhidi ya serikali yaliyopangwa kufanyika katika mji mkuu wa kibiashara Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA Freeman Mbowe alikamatwa mtaani, wakati naibu wake Tundu Lissu alikamatwa nyumbani kwake kufuatia mipango ya kuandamana kupinga mauaji na utekaji kwa wakosoaji wa serikali.
Watetezi wa haki za binadamu wanasema, serikali ya rais Samia Suluhu Hassan inawalenga wapinzani kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba na uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Hakuna maelezo ya haraka yaliyotolewa na serikali ya Samia Suluhu Hassan, ingawa awali ilisema inatetea demokrasia na haipuuzii ukatili.