Viongozi wa dini Kenya wawasihi wanasiasa kutoingilia shughuli za IEBC

kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo, cha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC.

Kundi la viongozi wa dini Kenya limewataka wanasiasa kujizuia kuiingilia kati Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)  mchakato wa kujumuisha matokeo ya kura.

Taasisi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki (KCCB) na Baraza la Taifa la Makanisa Kenya (NCCK) wanawasihi viongozi wa kisiasa kuipa IEBC muda na fursa kutekeleza jukumu lake la kikatiba.

Viongozi wa dini walikuwa wanazungumzia malumbano yaliyoripotiwa kati ya mawakala wa muungano wa Azimio na Kenya Kwanza siku ya Ijumaa katika Ofisi za Bomas ya Kenya, kituo cha kitaifa cha kujumuisha matokeo.

Tukiridhia kwamba taifa linaangalia uchaguzi wa rais, tumegundua kuwa sheria inamtaka mwenyekiti wa IEBC kuthibitisha na kujumuisha fomu za 34A,” alisema mchungaji Ferdinand Lugonzo, Katibu Mkuu wa KCCB katika taarifa iliyosomwa kwa pamoja na Mchungaji Chris Kinyanjui Kamau, Katibu Mkuu wa NCCK.

“Kama viongozi wa dini, tunapenda kutoa wito maalum kwa wagombea urais, mawakala wao na wafuasi wao wote, tafadhali endeleeni kutekeleza ahadi yenu ya amani na muwashawishi wafuasi wenu wawe na subira,” walisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ijumaa huko Karen, Donum Dei, jengo la Roussel House.

Wamewataka Wakenya waendeleze amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi.

“Kwa sababu hii, tunawasihi wakenya wote kuwa na subira. Hatakiwi mtu yeyote kufanya kitu kkitakacho hatarisha mshikamano wa kitaifa au kuwadhuru majirani zake.

Wachungaji hao walikuwa na wasi wasi juu ya ripoti za matukio ya wizi yaliyofanywa na kikundi cha maafisa wa IEBC, wakisema wale waliokutwa na makosa kila mmoja awajibishwe.

“Tumeona idadi ya maafisa wanaosimamia na kujumuisha matokeo wamekamatwa kwa shutuma za kujihusisha na matukio ya wizi wa kura. Kila afisa wa IEBC ni lazima waonywe kuwa atawajibishwa kila mmoja kwa vitendo vya uhalifu wanavyojihusisha navyo katika uchaguzi.