Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:49

Mbunge atafutwa na polisi kwa kumpiga risasi dereva wa mpinzani


Afisa wa polisi akilinda karatasi za kupiga kura kenya Aug 9 2022
Afisa wa polisi akilinda karatasi za kupiga kura kenya Aug 9 2022

Mbunge maarufu magharibi mwa Kenya Didmus Barasa anatafutwa na polisi kwa madai ya kumpiga risasi dereva wa mpinzani wake wakati wa zoezi la kuhesabu kura.

Barasa na mpinzani wake walikuwa wakifuatilia hesabu ya kura na mzozo ukazuka uliopelekea mpinzani wake kuondoka kwenye ukumbi.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Bungoma Joseph Ondoro amesema kwamba “Barasa alimfuata mpinzani wake aliyekuwa anaingia kwenye gari lake na kumuamuru aondoke kwenye kituo hicho lakini dereva wa mpinzani alikataa kuwasha gari na hapo ndipo Barasa akachomoa bastola na kumpiga risasi dereva.”

Madaktari walithibitisha kwamba amefariki alipowasili kwenye hospitali ya Kimilili.

XS
SM
MD
LG