Tutajadili hatma ya mpango wa kusafirisha nafaka tutakapokutana na Putin -Ramaphosa

PICHA YA MAKTABA: Rais Vladmir Putin wa Russia (Kushoto) na mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Mataifa ya Afrika yenye ushawishi yamesisitiza haja ya kuagiza nafaka, ili kukabiliana na uhaba wa chakula, wakati Rais wa Russia Vladimir Putin anajiandaa kujadili na viongozi wa bara hilo hatima ya makubaliano ya kuruhusu usafirishaji salama wa chakula na mbolea, kupitia  bahari ya Black Sea.

Putin amesema wiki hii kwamba Russia ilikuwa na nia ya kujiondoa kwa makubaliano ya usafirishaji wa nafaka kupitia Black Sea yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai mwaka jana kwa sababu "usafirishaji wake wa nafaka na mbolea bado unakabiliwa na vikwazo."

Mkataba huo huenda ukamalizika tarehe 17 mwezi Jualai mwaka huu.

Ujumbe wa viongozi wa Afrika unatarajiwa kuzuru nchini Ukraine na Russia kuanzia mwishoni mwa wiki hii katika harakati za kujaribu kumaliza vita vya muda mrefu vya miezi 16 vya Russia nchini Ukraine, na Putin amesema anapanga kutumia fursa hiyo kuzungumzia suala hilo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaamini kuwa Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wanakubaliana naye kuhusu "umuhimu wa kusafirisha nafaka barani Afrika kwa ajili ya kupunguza uhaba wa chakula," msemaji wa Ramaphosa Vincent Magwenya alisema.

"Kwa hivyo hatufahamu vitisho vyovyote vya kujiondoa katika mpango wa nafaka," Magwenya aliliambia shirika la habari la Reuters .

Naye Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kwamba Moscow bado haijafanya uamuzi wa kujiondoa.

Russia imetoa orodha ya matakwa ambayo inataka kutekelezwa, ikiwa ni pamoja na kurejesha mauzo yake yake ya kemikali ya amonia na kuunganishwa upya kwa Benki ya Kilimo ya Russia kwenye mfumo wa kimataifa wa malipo ya kupitia benki, wa SWIFT.

NARRATOR:

Putin amesema wiki hii kwamba Russia ilikuwa inafikiria kujiondoa kwa mpango wa nafaka wa Black Sea- uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai mwaka jana - kwa sababu usafirishaji wake wa nafaka na mbolea bado unakabiliwa na vikwazo.