Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:24

Rais wa Afrika Kusini kuchunguza madai ya Marekani, ya kuisaidia Russia


Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, atachunguza madai ya Marekani, kwamba meli ya Russia ilichikuwa silaha kutoka katika kambi ya wana maji karibu na CapeTown mwaka jana ofisi yake imesema Jumapili katika taarifa.

Afrika Kusini ilikanusha shutuma hizo ambazo zimesababisha malumbano ya kidiplomasia miongoni mwa Marekani, Afrika Kusini na Russia, na kuhoji msimamo wa Afrika Kusini wa kutoegemea upande wowote kwenye mgogoro wa Ukraine.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov amesema ahadi ya baadhi ya mataifa ya Magharibi kuipatia Ukraine ndege za kivita aina ya F-16, haikubaliki hata kidogo, na kuyashutumu mataifa hayo kwa kile alichokiita jaribio la kuidhoofisha Russia, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Russia.

Amekaririwa akisema kwamba hatua hiyo ni kucheza na moto kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG