Viongozi wa Afrika Kusini waeleza wasiwasi wa ghasia kuongezeka

Wafuasi wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakichoma matairi kuzuia magari kupita wakati wa maandamano huko Peacevale, Afrika Kusini, Julai 9, 2021.

Viongozi wa Afrika Kusini wanaeleza wasiwasi wao kutokana na kuongezeka kwa ghasia zilizoanza katika jimbo la Kwazulu-Natal.

Jimbo hilo ndiko anakotoka Rais wa zamani Jacob Zuma aliyeanza kifungo chake cha miezi 15 siku ya Jumatano ikiwa ni adhabu ya kukaidi amri ya mahakama.

Jumamosi usiku ghasia zimetokea katika vitongoji vya Alexandria na Jeppestown jijini Johannesburg ambako magari yamewashwa moto na madukwa kuporwa.

Maafisa wa usalama wanasema hawajui iwapo ghasia hizo za mji mkuu wa kibiashara zina husiana na kufungwa kwa Zuma.

FILE — Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiwa mahakamani huko Pietermaritzburg, Afrika Kusini, Jumatano Mei 26, 2021,

Kufuatana na taarifa ya polisi watu 62 wamekamatwa tangu Ijumaa, 37 katika jimbo la kwazulu Natal na 25 jijini Johannesburg kufuatia ghasia hizo.

Jumamosi jioni Rais Cyril Ramaphosa alitoa wito kwa watu kuwa watulivu, akiwataka waeleze hasira na maoni yao kwa utulivu wakizingatia sheria.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Rais pia amewataka wananchi kuepusha hali ya kuharibu mali jambo ambalo linaweza kuporomosha uchumi.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali