Zuma ambaye amehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 15 gerezani, uamuzi huo umeelezwa kuwa ni wa hasira na hauendani na katiba, kwa mujibu wa taasisi ya rais huyo wa zamani.
Mahakama ya Katiba, siku ya Jumanne ilimkuta Zuma na hatia ya kupuuza kufika mahakamani kusikiliza mashitaka ya rushwa yanayo mkabili.
Shutuma hizo zinatokana na makosa ambayo yalifanyika wakati akiwa madarakani.
Zuma amepewa siku tano kujisalimisha mwenyewe polisi.
Hata hivyo Jumatano usiku taasisi ya Jacob Zuma ilitoa taarifa ikisema wanasheria wake wataangalia namna ya kushughulikia shauri hilo kisheria.
Habari inatokana na vyanzo mbalimbali