Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:53

Biden na mkewe watembelea sehemu ya ajali Florida


Jengo la makaazi lililoanguka huko Surfside, Florida
Jengo la makaazi lililoanguka huko Surfside, Florida

Msemaji wa White House, Jen Psaki alisema Rais Biden na mkewe watakutana na wana familia ambao wamelazimika kuvumilia janga hili baya na vile vile kuwashukuru wahudumu waliofika kwanza kutoa msaada pamoja na timu ya uokozi

Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe wanasafiri Alhamis kwenda Surfside kwenye jimbo la Florida mahala ambapo timu za utafutaji na uokozi zinafanya kazi kwa siku ya nane mfululizo kwenye eneo lilipoanguka jengo la makaazi lenye ghorofa 12.

Maafisa wa eneo hilo walisema Jumatano kwamba idadi ya waliokufa kutokana na kuanguka kwa jengo iliongezeka hadi 18 wakiwemo watoto wawili. Msemaji wa White House, Jen Psaki alisema rais na mkewe watakutana na wana familia ambao wamelazimika kuvumilia janga hili baya na vile vile kuwashukuru wahudumu waliofika kwanza kutoa msaada pamoja na timu ya uokozi.

Timu ya utafutaji na waokozi ikiendelea na shughuli zake
Timu ya utafutaji na waokozi ikiendelea na shughuli zake

Msemaji wa White House alipoulizwa ikiwa Biden na mkewe wataenda kwenye eneo mahala jengo lilipoanguka alisema maelezo hayo bado hayajaamuliwa lakini rais alikuwa amesisitiza kwamba kila sehemu ya ziara yake inahitaji kuratibiwa na maafisa waliopo kwenye eneo.

Meya wa kaunti ya Miami-Dade, Daniella Levine Cava, alitangaza Jumatano kwa ku-tweet idadi ya watu waliopatikana hivi karibuni kutokana na kuanguka kwa jengo hilo la ghorofa na kwamba watu 145 bado hawajulikani walipo.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG