Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:35

Rais wa zamani wa Afrika kusini akubali kijasalimisha jela


Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma

Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma atajisalimisha kwa mamlaka husika ili aanze kutumikia kifungo cha miezi 15 jela kwa kuidharau mahakama.

Taasisi yake imesema ilimedhibitisha hilo Jumatano baada ya siku kadhaa ambapo wafuasi wake walizunguka nyumba yake wakizuia akamatwe. Mahakama ya katiba ilimuhukumu Zuma kifungo cha miezi 15 jela wiki iliyopita, kwa kukaidi amri ya mahakama hiyo mapema mwaka huu, ya kutoa ushahidi katika uchunguzi juu ya madai ya ufisadi wakati wa utawala wake wa miaka 9 uliomalizika mwaka wa 2018.

Taasisi ya Zuma imeandika kwenye ukurusa wake waTwitter “ rais Zuma ameamua kutii amri ya kifungo, yuko njiani kujisalimisha kwa mamlaka ya magereza ya KwaZulu Natal. Msemaji wa polisi Lirandzu Themba amethibitisha katika taarifa kwamba Zuma yuko katika jela la polisi, kwa kufuatisha uamzi wa mahakama ya katiba.

Zuma, mwenye umri wa miaka 79 alikua amepewa muda wa hadi Jumapili awe amejisalimisha. Polisi walikuwa wamepewa amri ya kumtia mbaroni mwishoni mwa Jumatano, iwapo atapinga kujisalimisha. Katika taarifa nyingine, mamlaka ya magereza imesema Zuma amefikishwa kwenye kituo cha mamlaka ya magereza, umbali wa kilomita 175 na makazi yake ya mji wa Nkandla.

Jibu la viongozi kwa mwenendo wa Zuma kukataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi baada ya miaka kadhaa ya madai ya ufisadi na uovu, imeonekana ni mtihani kwa Afrika kusini baada ya kipindi cha utawala wa ubaguzi wa rangi, kuweza kutekeleza sheria.

Zuma alikanusha kwamba kulikuwepo ufisadi uliokithiri chini ya uongozi wake, na Jumapili, alionyesha kitendo cha kukaidi, kwa kulinganisha majaji waliomuhukumu na wazungu walio wachache waliotawala enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi, ambao aliwahi kuwapiga vita.

XS
SM
MD
LG