Vikosi vya Tigray vyashambulia mji wa Bahir Dar kwa roketi

Mwanamke kutoka Ethiopia akita na watoto wake wakiwasili katika kambi ya wakimbizi ya Um-Rakoba katika mpaka kati ya Ethiopia na Sudan, katika jimbo la Al-Qadarif, Sudan, wakikimbia vita katika Jimbo la Tigray, Ethiopia, Novemba 19, 2020. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Wanajeshi wa jimbo la Tigray wamefyatua roketi katika mji wa Bahir Dar katika jimbo jirani la Amhara. Serikali ya amhara imesema hakukuwa na majeruhi wala uharibifu uliotokea. Wapiganaji wa chama cha Tigray liberation Front, TPLF wanapigana dhidi ya vikosi vya serikali. 

Siku ya Ijumaa TPLF wamewatuhumu wanajeshi wa serikali kwa kushambulia chuo kikuu cha Mekele na kuwajeruhi idadi fulani ya wanafunzi. Serikali ya Addis Ababa haijatoa taaifa yeyote kuhusiana madai hayo.

Wakati huo huo Mkuu ya jeshi la Anga la Ethiopia Yilma Merdasa amekiri kwamba wanatumia ndege zisizo na rubani katika mapigano huko Tigray lakini kukanusha madai kwamba ndege hizo zinatoka nchi za nje.

Serikali ya Jimbo la Amhara ambalo kwa muda mrefu limekuwa na mgogoro wa mpaka na wakuu wa Tigray imetuma wapiganaji wake kusaidia wanajeshi wa serikali.

Mamia ya watu wamekufa katika ghasia kwenye jimbo la Tigyari tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba na zaidi ya watu 30,000 wamevuka mpaka kutoka Ethiopia kuingia sudan kutafuta hifadhi wakiohofia maisha yao.