Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:26

Viongozi wa Afrika waanza juhudi za kutafuta suluhu mgogoro wa Ethiopia


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Viongozi wa nchi za Afrika wameanza Jumatatu juhudi za kutafuta suluhisho kwa mzozo unaozidi kuongezeka nchini Ethiopia, siku mbili baada ya roketi kushambulia mji mkuu wa Eritrea na kuzusha hofu kwamba ugomvi huwenda ukaenea. 

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana na naibu waziri mkuu, ambae pia ni waziri wa mambo ya nje wa Ethopia, Demeke Mekonnen hii leo mjini Gulu, Kaskazini mwa Uganda, kuzungumzia hali ya huko Tigray.

Naye rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo anaelekea Addis Ababa katika juhudi za kuanzisha majadiliano.

Kwenye uwanja wa mapigano, serikali ya Ethiopia imetangaza Jumatatu kwamba ndege zake zimeshambulia vituo vya kijeshi kwenye mji mkuu wa Tigray wa Mekele baada ya kutangaza kwamba wanajeshi wa serikali wamekomboa miji kadhaa ikiwa ni pamoja na miji mkubwa ya Waja na Alamata.

Wakuu wa serikali ya Tigray wamethibitisha mashambulizi hayo lakini kudai kwamba mashambulizi ya ndege yalilenga maeneo ya raia.

Wakati huo huo Sudan imetoa wito kwa jumuia ya kimataifa kusaidia kukabiliana na wakimbizi wanaokimbia mapigano katika jimbo la Tigray wanaoingia mashariki mwa nchi.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limeripoti kwamba karibu wakimbizi elfu 25 walokua na nja na kuchoka wameingia Sudan na kuonya uwezekano wa kuzuka janga la kibinadamu huko.

XS
SM
MD
LG