Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:18

Wapiganaji wa Tigray washambulia viwanja vya ndege uhasama ukiongezeka Ethiopia


Wanamgambo wa kiamhara wanaounga mkono wanajeshi wa serikali kuu wanaopigana katika jimbo la kaskazini la Tigray.
Wanamgambo wa kiamhara wanaounga mkono wanajeshi wa serikali kuu wanaopigana katika jimbo la kaskazini la Tigray.

Serikali ya jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia imetangaza Jumamosi kwamba mashambulio ya makombora ndani ya jimbo la Amhara ni ulipizaji kisasi wa mashambulio ya ndege yaliyofanywa na jeshi la serikali kuu jimboni humo hivi karibuni. 

Serikali ya Addis Ababa ilitoa taarifa Jumamosi ikieleza kwamba roketi mbili ziliharibu sehemu ya uwanja wa ndege wa Gondar jimboni Amhara, Ijuma usiku na mmoja ikikosa shabaha yake kwenye uwanja wa ndege wa Bahir Dar.

Jeshi la Ethiopia limekua likipambana na wapiganaji wa jimbo hilo kwa zaidi ya wiki moja na inaripotiwa mamia ya watu wamefariki tangu waziri mkuu Abiy Ahmed kupeleka majeshi huko hapo Novemba 4.

Mapigano yamewasababisha maelfu ya watu kukimbia katika nchi jirani ya Sudan na Eritrea wakidai kuwepo na mateso na hali ya wasi wasi.

Mkuu wa kimkoa wa idara ya wakimbizi ya Sudan, Alsir Khaled amesema Ijuma kwamba kuna waethopia elfu 21 walovuka mpaka, wengi vijana, walikua na njaa na wamechoka baada kutembea kwa siku kadhaa.

Kamishna wa haki za binadam wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameeleza Ijuma jinsi alivyoshtushwa na namna hali ilivyozorota haraka huko Tigray.

Msemaji wake Rupert Colville anasema, Bachelet amekerwa zaidi na ripoti ya Shirika la haki za binadam la Amnesty Internationl kuhusu tuhuma za mauwaji ya halaiki huko Mai-Kadra kusini magharibi mwa Tigray.

Bachelet ameonya kwamba huwenda kuna uhalifu wa vita umetengdeka huko Tigray .

XS
SM
MD
LG