Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:29

Mkurugenzi wa WHO Ghebreyesus ashutumiwa kusaidia chama cha TPLF kupata silaha


Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Jeshi la Ethiopia leo limemshtumu mkurungenzi wa shirika la afya duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus kukiunga mkono chama tawala cha TPLF katika jimbo la Tigray, kwa kujaribu kutoa msaada wa silaha na kidiplomasia kwa chama hicho.

Tedros amekanusha kupendelea upande wowote katika ugomvi huo akitoa wito kwa pande zote kufanya kazi kurudinha amani na usalama wa raia.

Kwenye ujumbe wa Twitter, Tedros amesema, "Kumekuwepo na ripoti zinazosema mimi ninapendelea upande moja wa ugomvi huu. Hiyo sio kweli na nina taka kusema kwamba mimi niko upenda moja tu, na upande huo ni upande wa amani."

Tedros, mwenye asili ya Tigray, aliwahi kuhudumu kwenye serikali ya ushirika ya Ethiopia iliyokua inaongozwa na chama cha TPLF kama waziri wa afya na waziri wa mambo ya nje kati ya mwaka wa 2005 na 2016.

Chama cha TPLF kiliongoza Ethiopia kikiwa chama chenye nguvu kwa miongo kadha, hadi waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipochukua madaraka miaka miwili iliopita.

Mkuu wa majeshi ya Ethiopia Berhanu Jula akizungumza na waandishi habari Alhamisi, amemtuhumu mkurugenzi wa WHO, kwa kukiunga mono chama cha TPLF na kukitafutia silaha.

"Hivi sasa kutokana na wenzake ambao wana mawazo sawa, wanaungana pamoja, unatarajia nini kutoka kwake. Sisi hatukutajaria kamwe ataungana na watu wa Ethiopia ili kuwalaani hao wengine,” amesema Berhanu.

XS
SM
MD
LG