Chini ya makubaliano yaliyosaininiwa Alhamisi nchini Uturuki, makubaliano hayo ni kuboresha maendeleo ya pande mbili , kisayansi, kiteknolojia na ushirikiano wa kibiashara kati ya Uturuki na Somalia katika kuendeleza mafuta na gesi ya Somalia, kulingana na waziri wa Petroli na mali asili, Abdirizak Mohamed.
Mohamed amesema Uturuki itatafuta mafuta na gesi nchini Somalia, kote ufukweni na baharini.
Mohamed amesema mpango huo ni moja ya itifaki za Mkataba wa Mfumo wa Ushirikiano wa Kiuchumi uliofikiwa na nchi hizo mbili mwezi uliopita.
Chini ya makubaliano hayo, ambayo yatadumu kwa miaka 10, Uturuki itajenga, kutoa mafunzo na kilipatia vifaa jeshi la wanamaji la Somalia, kulingana na waziri mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre.
Waziri huyo wa petroli na mali ya asili amesema mkataba utakaofuata utakuwa na maelezo ya kushirikiana uzalishaji pamoja na ratiba ya makubaliano.