Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:59

Uturuki kuipa Somalia msaada wa ulinzi wa baharini


Meli ya uvuvi ya Iran iliyokuwa imetekwa nyara na maharamia katika pwani ya Somalia. Picha na INDIAN NAVY / AFP.
Meli ya uvuvi ya Iran iliyokuwa imetekwa nyara na maharamia katika pwani ya Somalia. Picha na INDIAN NAVY / AFP.

Uturuki itaipatia Somalia ulinzi wa baharini kuisaidia nchi hiyo ya Afrika kuyalinda maeneo yake ya majini, afisa wa wizara ya Ulinzi ya Uturuki amesema siku ya Alhamisi.

Uturuki na Somalia mapema mwezi huu wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi na uchumi wakati waziri wa ulinzi wa Somalia alipoitembelea Ankara.

Akitoa maoni yake kuhusu mkataba huo, afisa wa wizara ya ulinzi ya Uturuki akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake amesema, Ankara imekuwa ikitoa mafunzo kwa jeshi la Somalia kwa zaidi ya miaka kumi.

Makubaliano yanalenga kuimarisha ushiriano wa ulinzi kati ya Uturuki na Somalia, afisa huyo amesema.

“Kutokana na ombi la Somalia, tutatoa misaada katika eneo la ulinzi wa majini, kama tulivyofanya katika maeneo ya mapmbano dhidi ya ugaidi,” alisema.

“Tutaisaidia Somalia kukuza uwezo wake wa kupambana na vitendo haramu na harakati zisizo za kawaida katika eneo lake la maji yake.”

Uturuki imekuwa ni mshirika wa karibu wa serikali ya Somalia katika miaka ya hivi karibuni. Ankara imejenga shule, hospitali na miundombinu na imetoa nafasi za masomo kwa Wasomali kwenda kusoma Uturuki.

Chanzo Cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG