Mahakama ya juu ya Israel imekubaliana na amri ya serikali kwamba Omar Shakir ambaye ni mkurugenzi mkazi wa HRW nchini Isreal na Palestina ni lazima aondoke nchini humo Jumatatu.
Israel pia imewanyima hati za kuingia nchini watu wengine mashuhuri wanaosemekana kuunga mkono vuguvugu hilo wakiwemo wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa hii ni mara ya kwanza kwa afisa wa HRW aliyeko ndani ya nchi kuamriwa kuondoka.
Shakir amesema kuwa hatua iliyo chukuliwa dhidi yake inathibitisha ukandamizaji wa haki za binadamu unaotekelezwa na utawala wa Netanyahu.
Amesema ukandamizaji huo umekuwa ukiwaathiri watu wengi wakiwemo wanafunzi wa kigeni kwenye vyuo vikuu pamoja na jamii za watu wanaoikosoa serikali pamoja na wanaharakati.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.