Akikutana na katibu mkuu wa NATO Mark Rutte mjini Brussels, Blinken pia alisema kupelekwa vikosi vya Korea Kaskazini kwa ajili ya kuisaidia Russia katika vita vya Ukraine kutopata jibu thabiti.
Blinken aliwaambia waandishi wa habari kuwa uhusiano wa Moscow na Pyongyang “ulikuwa wa pande mbili” na kuna wasiwasi mkubwa kuhusu kile ambacho Russia inafanya au inaweza kufanya ili kuimarisha uwezo wa Korea Kaskazini ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa nyuklia.
Rais mteule Donald Trump ambaye aliwahi kuhoji msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine, alisema atamaliza haraka vita vya Russia bila kueleza zaidi, ambapo ilizusha wasiwasi miongoni mwa washirika wa Marekani kwamba atajaribu kuilazimisha Kyiv kukubali amani kwa masharti ya Moscow.
Biden anaondoka madarakani Januari 20.