Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 09:33

Ukraine imeishambulia Moscow kwa kutumia Drone angalau 34


Mfano wa Drone za Ukraine ambazo zimetumika kuishambulia Moscow.
Mfano wa Drone za Ukraine ambazo zimetumika kuishambulia Moscow.

Idara ya usafiri wa anga ya Russia lilisema viwanja vya ndege vya vitatu vilibadilisha mwelekeo wa angalau safari za ndege 36

Ukraine iliishambulia Moscow leo Jumapili kwa ndege zisizokuwa na rubani-Drone angalau 34, shambulio kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani katika mji mkuu wa Russia tangu kuanza kwa vita hivyo mwaka 2022, na kuzilazimisha ndege ubadili safari zake kutoka viwanja vya ndege vikubwa vitatu katika mji huo na kumjeruhi angalau mtu mmoja.

Ulinzi wa anga wa Russia uliharibu Drone nyingine 36 kwenye mikoa mingine ya magharibi mwa Russia katika muda wa saa tatu leo Jumapili, wizara ya ulinzi imesema.

Jaribio lililofanywa na utawala wa Kyiv kufanya shambulio la kigaidi kwa kutumia ndege zisizo na rubani katika eneo la Shirikisho la Russia lilizuiwa, wizara hiyo ilisema.

Idara ya usafiri wa anga ya Russia lilisema viwanja vya ndege vya Domodedovo, Sheremetyevo na Zhukovsky vilibadilisha mwelekeo wa angalau safari za ndege 36, lakini baadaye zilianza tena shughuli zake. Mtu mmoja aliripotiwa kujeruhiwa mjini Moscow.

Forum

XS
SM
MD
LG