Takwimu kutoka mradi unaojulikana Armed Conflict Location and Event Data umebaini kuwa ghasia nchini Burkina Faso, Mali na Niger zimesababisha zaidi ya vifo 4,660 katika muda wa miezi sita ya kwanza ya mwaka 2020.
Takwimu kutoka makundi mengine ya kimataifa yanayofuatilia na mashirka ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa ukosefu wa makazi ndani ya nchi katika eneo la kati la Sahel huko Afrika umeongezeka mara kumi tangu mwaka 2013, kutoka 217,000 mpaka milioni 2.1 mwishoni mwa mwaka 2021.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, Boris Cheshirkov anasema ukosefu wa makazi unaendelea huko Sahel, wakati raia wakikimbia mashambulizi, “makundi yenye silaha yameripotiwa katika mashambulizi mabaya zaidi ya 800 mwaka jana.
Ghasia kama hizo zimewabandua watu 450,000 ndani ya nchi zao na kuwalazimisha takriban 36,000 kukimbilia nchi jirani kama wakimbizi. Wanawake na watoto mara nyingi wanaathiriwa vibaya sana na mashambulizi na kujikuta katika mazingira hatarishi na manyanyaso ya kijinsia,” ameongezea.
Cheshirkov anasema hali kote katika eneo hilo inaendelea kuzorota. Anasema jamii wenyeji na maafisa wa serikali wanajitahidi kuongeza shinikizo licha ya nia yao ya dhati kuwasaidia watu wasiokuwa na makazi.
Anasema mashirika ya kibinadamu yanakumbana na ugumu mkubwa na hali ya hatari katika kusambaza misaada na kutoa ulinzi. Anasema mashirika hayo yako katika hatari ya kukumbwa na mashambulizi ya barabarani, kuvamiwa na kutekwa kwa magari yao.
“Tulichokuwa tunakiomba kila mara na tunaendelea kukisema ni hivi sasa kuungana, kuwa na mkakati, ungiliaji kati wenye tija katika Sahel hatua ambazo zitahakikishwa kwamba juhudi za kimataifa zinazisaidia serikali na jamii wenyeji na majibu ya usalama hayawezi kushinda kipekee. Kunahitajika juhudi za kibinadamu ziende sambamba na hatua za maendeleo,” amesema Cheshirkov.
Anasema UNHCR inaongoza juhudi za Umoja wa Mataifa na mashirika binafsi ili kutoa makazi na huduma za ulinzi, ikiwemo kupambana na manyanyaso ya kijinsia.