Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:12

Idadi ya raia wa Cameroon wanaokimbia ghasia yaendelea kuongezeka


Hema la UNHCR katika kambi ya wakimbizi Djibouti (Picha AP/Mosa'ab Elshamy)
Hema la UNHCR katika kambi ya wakimbizi Djibouti (Picha AP/Mosa'ab Elshamy)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linasema idadi ya raia wa Cameroon wanaokimbia ghasia kaskazini mwa nchi na kuingia nchi jirani ya Chad inaendelea kuongezeka.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linasema idadi ya raia wa Cameroon wanaokimbia ghasia kaskazini mwa nchi na kuingia nchi jirani ya Chad inaendelea kuongezeka. Cameroon imepeleka ujumbe nchini Chad kuwashawishi wale waliokimbia mapigano juu ya mzozo wa vyanzo vya maji kurejea nyumbani.

UNHCR inasema watu hao ambao wamekimbia mapambano ya kikabila mwezi huu imeongezeka na kufikia 82,00.

Mapigano yalizuka kwenye Kijiji cha mpakani cha Ouloumsa nchini Cameroon wiki mbili zilizopita kati ya wafugaji ng’ombe wa Arab Choua na wavuvi wa kabila la MOusgoum, wakisababisha maelfu ya watu kukimbilia nchini Chad.

Maafisa wa Cameroon wamesema mapambano juu ya rasilimali za maji zimeviacha vijiji na masoko yakiwa yamechomwa moto, mazao kuharibiwa, na mifugo kuuliwa au kuibiwa.

Mwakilishi wa UNHCR nchini Chad, Papa Kysma Sylla, anasema haja ya raia kukimbia inazidi kuongezeka kila siku.

“Tuko katika hali ya dharura iliyotangazwa wazi wazi kutoka makao makuu yetu, kwahiyo tumeunda uratibu na NGOs kadhaa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile WFP, UNICEF, Msalaba Mwekundu. Kwahiyo, tunatoa misaada na fedha au rasilimali za kibinadamu,” anasema Sylla.

Mahamat Kerimo Sale, mayea wa wilaya ya 9 mjini N’djamena nchini Chad, aliiambia VOA kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwamba rais wa baraza la kijeshi la mpito la Chad, Mahamat Deby, ametoa maagizo kwa raia wa Chad kwa amani kuwakaribisha watu wanaokimbia mizozo nchini Cameroon. Anasema wanatoa huduma zaz msingi kama vile chakula na maji na mashirika ya misaada na yale y a Umoja wa mataifa kama UNICERF pia yanasaidia kwa kugawa sabuni na mablanketi ili kupunguza madhila kwa wale ambao wamekoseshwa makazi nchini Cameroon.

Sale anasema baadhi ya wale wanaotoka katika jamii zinazopigana waliokimbia Cameroon wamewekwa peke yao ili kuepuka mzozo nchini Chad.

Serikali ya Cameroon wiki iliyopita ilipeleka ujumbe nchini Chad kuwasaidia wale ambao wamekimbia ghasia.

Waziri wa utawala wa eneo Paul Atanga Nji aliongoza ujumbe wa mawaziri, maafisa wa kijeshi na wabunge.

Nji aliishukuru serikali ya Chad na watu wake kwa kuwapatia huduma wacameroon wasiokuwa na makazi.

Pia aliwaomba wale waliokimbia makazi yao kurejea nyumbani nchini Cameroon na kuimarisha amani na jirani zao.

“Ingawaje tunasisitiza amani, umoja, utulivu na kuisha pamoja, pia tunajaribu kuielewesha jamii kwamba si vizuri kuchukua sheria mikononi mwao na kwamba kama kuna tatizo lolote, ni vyema waende kwa maafisa wa karibu au vyombo vya sheria na kulalamika. Kwasababu kama kuna matatizo kati ya wafugaji au maeneo ya malisho na wakulima, kuanza kuuwana na kuiba vitu, nadhani siyo mfano mzuri. Tuko katika utawala wa sheria.” Amesema Nji.

Nji anasema hadi hivi sasa, raia 6,000 wa Cameroon ambao walikimbilia Chad wamekubali kurejea nyumbani.

Maafisa wa Cameroon wanasema wamepeleka wanajeshi kwenye maeneo yenye mzozo ili kuhakikisha usalama kwa raia wote.

XS
SM
MD
LG