UN yasema wanawake wanawakati mgumu wa kupata ajira ulimwenguni hivi sasa kuliko siku za nyuma

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Umoja wa Mataifa umesema wiki hii kwamba wanawake wamekuwa na wakati mgumu wa kupata fursa za kazi ulimwenguni kuliko ilivyodhani hapo awali.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterress ameeleza hayo na kuongeza kuwa mwanya wa jinsia katika hali makazini na malipo haujabadilika sana katika kipindi cha miongo miwili, wakati dunia ikisherehekea siku ya kimataifa ya wanawake.

Guterres alionya Jumatatu kwamba maendeleo ya ulimwengu kuhusu haki za wanawake yanapotea mbele ya macho yetu, akisema kuna ongezeko kubwa mwanya katika usawa wa jinsia ambapo huenda ikachukua karne tatu kufanikisha hayo.

Usawa wa jinsia unazidi kuwa na mwanya mkubwa. Kwa mwenendo wa sasa, idara ya UN Women inauweka uko bali kwa miaka 300, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kwenye hotuba yake kabla ya siku ya kimataifa ya wanawake leo Machi 8, wakati alipokuwa akizindua majadiliano ya wiki mbili yanayoongozwa na tume ya hadhi ya wanawake.

Kwa mwenendo wa sasa, UN Women unauweka umbali kwa miaka 300. Ongezeko la vifo vya kina mama waja wazito. Mwanamke mmoja anafariki kila dakika mbili wakati wa uja uazito na kujifungua. Vifo vingi vinaweza kuzuilika. Matokeo ya janga la Covid 19 yanaendelea kwa mamilioni ya wasichana waliolazimika kuacha shule, kina mama na watoa huduma wamelazimika kuacha kazi za kulipwa na watoto wametumbukizwa katika ndoa za mapema. Kuanzia Ukraine mpaka Sahel, mizozo na migogoro inawaathiri wanawakena wasichana kwa kiwango kibaya sana. Na katika kiwango cha kimataifa, baadhi ya nchi hivi sasa zinapinga kujumuishwa kwa dhana ya jinsia katika mashauriano mbali mbali,” amesema Guterres.

Wanawake wakisherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake

Aliangazia hasa hali mbaya huko Afghanistan ambayo inatawaliwa na Taliba, ambako wanawake na wasichana wametolewa katika maisha ya umma.

Hakutaja nchi nyingine kwa majina, lakini Guterres alisisitiza kwamba “katika sehemu nyingi, wanawake haki ya uzazi zimerudishwa nyuma katika baadhi ya nchi, wasichana wanaokwenda shule wako katika hatari ya kutekwa na kushambuliwa.

Guterres aliongezea kwa kifaransa kwamba mundo ya kazi kimataifa haifanyi kazi kwa dunia ya wanawake na wasichana na kusisitiza haja ya mabadiliko. “Ni vyema tuwe wazi. Miundo ya kazi kiamtaifa haifanyi kazi kwa ajili ya wanawake na wasichana duniani. Kuna haja ya mabadiliko. Juhudu zangu ni kuchochea malengo ya maendeleo endelevu yawe katika njia sahihi na kuwepo kwa mageuzi katika mfumo wa kifedha ulimwenguni wenye lengo la kuongezea uwekezaji kwa wanawake na wasichana katika kiwango cha nchi.”

Shirika la kimataifa la kazi duniani ILO limesema limeweka viashiria vipya ambavyo vinafanya kazi nzuri kuliko viwango rasmi vya ukosefu wa ajira katika kufahamu watu wote ambao hawana ajira na wanajitahidi kutafuta kazi.

Inaonyesha picha ambayo si nzuri kwa hali ya wanawake katika dunia ya kazi kuliko ili iliyozoeleka inayotumiwa ya kwiango cha ukosefu wa ajira, taarifa ya ILO ilisema Jumatatu.

Kwa mujibu wa data mpya za ILO, asilimia 15 ya wanawake walio na umri wa kufanya kazi duniani wangependa kuwa kazini, lakini hawana ajira, ukilinganisha na asilimia kumi na nusu ya wanaume.

Mwanya huu wa jinsia bado haujabadilika kwa miongo miwili, ilisema taarifa.

Shirika hilo la kazi la Umoja wa Mataifa limegundua kwamba mwanya wa kajira ulikuwamkubwa sana katika nchi zenye kipato cha chini, ambako karibu robo ya wanawake wanashindwa kupata kazi.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Serbia.

Viwango rasmi vya ukosefu wa ajira kwa wanawake na wanaume viko karibu sawa.

Hii ILO inasema ni kwasababu ya kigezo kilichotumiwa kuangalia kama kuna mtu ambaye anatakiwa kufikiriwa kuwa hana ajira lakini bila ya uwiano kimewaengua wanawake.

Katibu Mkuu amesema “lengo lenu mwaka huu ni juu ya kuziba mianya katika teknolojia na ubunifu na hali limekuja wakati muafaka. Kwasababu wakati teknolojia inazidi kusonga mbele, wanawake na wasichana wameachwa nyuma. Hesabu yake ni rahisi. Bila ya maaria na ubunifu wa nusu ya dunia, sayansi na teknoloji zitakidhi nusu ya matarajio. Watu bilioni tatu bado hawana huduma ya internet, lakini wengi wao ni wanawake na wasichana katika nchi zinazoendelea.”

Guterres ametaka hatua za pamoja kote duniani zichukulie na serikali, jamii za kiraia na sekta binafsi kutoa elimu inayojibu masuala ya jinsia, kuboresha mafunzo ya ujuzi na kuwekeza zaidi katika kuziba mgawanyiko wa jinsia kidigitali.