Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:12
VOA Direct Packages

UN yasema utapiamlo umeongezeka kwa asilimia kubwa miongoni mwa wanawake wajawazito


Picha ya wanawake wa kiafrika kwenye makazi duni
Picha ya wanawake wa kiafrika kwenye makazi duni

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba utapiamlo umekithiri miongoni mwa wanawake wajawazito pamoja na wale wananaonyonyesha.

Hali hiyo inasemekana kuongezeka kwa asilimia 25 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, katika mataifa 12 yalioathiriwa na kupanda kwa bei za vyakula kutokana na vita vya Ukraine. Utafiti kwenye mataifa 10 ya kiafrika na mawili ya Mashariki ya Kati, ambayo yameathiriwa zaidi umetumika kwenye ripoti hiyo ya UNICEF ya Jumanne, kabla ya maadhimisho ya Jumatano, ya siku ya kimataifa ya wanawake.

Ripoti imeongeza kusema kwamba ukosefu wa lishe bora miongoni mwa wajawazito na wale wanaonyonyesha huenda ukapelekea kushuka kwa kinga dhidi ya maradhi, pamoja na matatizo wakati wa kujifungua. Baadhi ya mataifa yaliyopo chini ya jangwa la Sahara yameonyesha kuwa ni viwango vya juu vya vifo vya watoto wa kuzaliwa kwenye tafiti za awali, vikisababishwa na matatizo mbalimbali.

Takriban watoto milioni 51 waliopo chini ya umri wa miaka miwili kote ulimwenguni ni wafupi kuliko wanavyofaa kuwa kwa umri wao, kutokana na utapiamlo, na nusu yao huathiriwa wakiwa tumboni au katika miezi 6 ya kwanza ya maisha.

Wasichana walioathiriwa wameongezeka kutoka milioni 5.5 mnamo mwaka wa 2020 hadi milioni 6.9 mwaka jana, katika nchi kama Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Somalia, South Sudan, Sudan, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

XS
SM
MD
LG