Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 12:06

Jill Biden asifu Namibia kwa juhudi zake kwelekea usawa wa kijinsia


Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akipungia mkono, wakati akipokaribishwa na mke wa rais wa Namibia Monica Geingos, kabla ya kuzungumza katika hafla ya chakula cha mchana kwenye makazi ya rais wa Namibia huko Windhoek, Namibia, Feb. 23, 2023.
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akipungia mkono, wakati akipokaribishwa na mke wa rais wa Namibia Monica Geingos, kabla ya kuzungumza katika hafla ya chakula cha mchana kwenye makazi ya rais wa Namibia huko Windhoek, Namibia, Feb. 23, 2023.

Mke wa rais wa Marekani Jill Biden, ambaye yuko ziarani nchini Namibia, amesifu utawala wa Rais wa nchi hiyo, Hage Geingob, kwa hatua zilizopigwa katika juhudi za kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia serikalini.

Bi Biden alikuwa akitoa hotuba yake wakati wa dhifa ya chakula cha mchana, iliyoandaliwa na Rais wa Namibia na mkewe mjini Windhoek,.

Tayari nimeona jinsi unavyoongoza hapa Namibia. Unavyotilia maanani usawa wa kijinsia.

"Serikali yako imejaa wanawake wenye nguvu. Ni mfano wa kuigwa na ulimwengu," alisema Biden.

Ameongeza kuwa Marekani imejitolea kuhakikisha kuwa nchi za Kiafrika hazipati tu, sauti katika mashirika kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na G20, lakini sauti hizo zinathaminiwa kama washirika sawa, na kwamba utawala wa Biden utafanya kazi bega kwa bega ili kuendeleza vipaumbele vya pamoja, kkama vile kuwawezesha wanawake na vijana, kuimarisha afya duniani, na kujenga ustawi wa kiuchumi.

Bi Biden pia alitarajiwa kutembelea mradi unaofadhiliwa na Marekani katika mji mkuu, Windhoek, ambao unalenga katika kuwawezesha wanawake na watoto na kuhakikisha upatikanaji wa fursa za kiuchumi na rasilimali za afya.

Baada ya kuwasili nchini humo jana Jumatano, Biden alisema Namibia ilichaguliwa kutokana na kunawiri kwake katika nyanja mbalimbali. Jill Biden ndiye afisa wa kwanza wa Ikulu ya Marekani kuzuru nchi hiyo baada ya Rais Joe Biden mwaka jana kuahidi kutuma maafisa wa utawala katika bara hilo.

Anamfuata Waziri wa Fedha Janet Yellen na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, waliotembelea mapema mwaka huu. Ziara ya Jill Biden, pia itampeleka Kenya hapo kuanzia Ijumaa.

Biden pia alitarajiwa kuutembelea mradi unaofadhiliwa na Marekani katika mji mkuu Windhoek, mradi ambao unalenga kuwawezesha wanawake na watoto na kuhakikisha wanapata fursa za kiuchumi za kiuchumi na rasilimali za afya.

Baada ya kuwasili nchini humo siku ya Jumatano, Biden alisema Namibia imechaguliwa kwa sababu jins inavyonawiri.

“Tulikata kuja kwa sababu tunajua hii ni nchi yenye kidemokrasia changa, na tunataka kuunga mkono demokrasia duniani kote” alisema Biden.

“Tulikutana Desemba na tunaendeleza uhusiano. Nadhani ni sahihi mimi na Monica kusema tumekuwa marafiki wazuri kwa haraka,” alisema.

Geingos alisema kuna mengi nchini Namibia ambayo angependa kumuonyesha mke wa rais wa Marekani ambaye amefanya ziara yake ya kwanza nchini humo.

“Ni nchi yenye demokrasia iliyonawiri. Tuna idadi kubwa ya vijana ambao wanasukuma demokrasia, wenye juhudi za hali ya juu na wanawezeshwa kikamilifu na thamini za katiba yetu na pia maadili binafsi ya uongozi wetu” Geingos alisema.

Jill Biden ni afisa wa kwanza wa White House kuitembelea nchi hiyo, baada ya rais Joe Biden mwaka jana kuahidi kutuma maafisa wa utawala barani Afrika. Ziara ya Jill Biden inafuatia ziara ya waziri wa fedha Janet Yellen na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield, walioitembelea nchi hiyo mapema mwaka huu.

Jill Biden anaelekea Kenya, ambako atatumia umaarufu na jukwaa lake kuhamasisha masuala ya uwezeshaji wa wanawake na watoto na janga la njaa ambalo pia linasababisha tena maafa katika eneo hilo la Pembe ya Afrika.

XS
SM
MD
LG