Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:17

Kenya kuchunguza tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwenye mashamba ya chai


Mwanamke akichuma chai katika shamba lililoko huko Nandi Hills, Magharibi mwa mji mkuu Nairobi, Nov. 5, 2014.
Mwanamke akichuma chai katika shamba lililoko huko Nandi Hills, Magharibi mwa mji mkuu Nairobi, Nov. 5, 2014.

Wabunge nchini Kenya wanasema watachunguza tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwenye mashamba ya chai ambayo baadhi yao huzisambaza chapa maarufu nchini Uingereza.

Zaidi ya wanawake 70 wanaofanya kazi katika mashamba yaliyoko katika eneo la Rfit Valley nchini Kenya walimwambia mwandishi wa habari wa siri w BBC aliyekuwa akichunguza habari hiyo iliyodai wanawake hao walikuwa wamenyanyaswa kingono na wasimamizi wao wa kazi kwa miaka mingi.

Makala hiyo iliyoonyeshwa wiki hii ilizua taharuki nchini Kenya, moja ya wauzaji wakubwa wa chai duniani.

Mwakilishi wa wanawake wa Kaunti ya Kericho, Beatrice Kemei, ambaye eneo bunge lake linajumuisha maeneo yenye mashamba ya chai, Jumanne alitoa wito wa “haraka” kwa wahusika wafunguliwe mashtaka.

Kemei alisema kuwa aliiangalia makala hiyo "kwa mshtuko mkubwa na kutoamini" amelaani "kitendo (vitendo) vya ukatili kwa matamshi makali sana".

"Lazima tuungane kutetea ulinzi wa wanawake dhidi ya matendo maovu kama haya yanayo wadhalilisha," aliliambia bunge.

Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Jane Marriott, alisema Jumatano kwamba ana wasi wasi na "tabia hii ya kutisha", na kuongeza kuwa "unyonyaji hauna nafasi katika jamii."

Makala hiyo iliangazia kwenye shamba moja la Kenya ambalo wakati huo lilikuwa linamilikiwa na kampuni kubwa ya chai ya Unilever ya Uingereza, na nyingine inayomiliwa na makampuni ya James Finlay & Co.

Chanzo cha habari hii ni Agence France-Presse AFP

XS
SM
MD
LG