UN yaitaka Sudan Kusini kuharakisha utekelezaji wa mkataba wa amani wa 2018

Viongozi wa Sudan Kusini.

Afisa wa ngazi ya juu zaidi wa  Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jumanne aliwataka viongozi wa taifa hilo kuharakisha utekelezaji wa mkataba wa amani wa mwaka 2018, ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2024.

"Sasa si wakati wa kuondoa macho yetu Sudan Kusini," Nicholas Haysom, mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. "Tunachoweza kujifunza kutoka kwa Sudan ni jinsi mafanikio ya amani yaliyopatikana kwa bidii yanaweza kusambaratika," aliongeza.

Huu ni mwaka muhimu kwa nchi hiyo. Katiba mpya lazima iandaliwe na matayarisho yakamilishwe kwa uchaguzi wa kwanza wa kitaifa uliopangwa kufanyika mwezi Disemba mwakani.

"Katika makadirio yetu, mchakato wa kutengeneza katiba umechelewa kwa muda wa miezi 10, upangaji wa uchaguzi miezi minane, na vipengele kadhaa vya mipango ya mpito ya usalama havina msingi thabiti," Haysom aliripoti.

Alisema inawezekana kwa Sudan Kusini kuziba pengo la maandalizi ya uchaguzi, na kuwataka wabunge kupitisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi bungeni na kuunda Tume ya Taifa ya Uchaguzi.