Zaidi ya watu laki saba wamekimbia kupitia kivuko cha mpakani cha Joda katika kipindi cha miezi 21 iliyopita wakati maelfu ya watu wengine wamevuka na kuingia Sudan Kusini na kwingineko.
Wimbi hili la wakimbizi limefikisha jumla ya idadi ya watu waliokimbia kufikia zaidi ya milioni moja kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa.
Mamilioni ya watu wengi wanaovuka mpaka ni raia wa Sudan Kusini ambao awali walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo changa, shirika la kuhudumia wakimbizi la UNHCR limesema katika taarifa yake.
Taarifa ya Pamoja ya UN imetoa wito wa kuongezwa misaada zaidi kwa watu wote waliokoseshwa makazi na watu wanaowahifadhi , wakionya kwamba rasilimali za sudan kusini kama vile huduma za afya , maji na makazi zimetumika sana .