Watu wanne waliuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika shambulizi la Jumapili lililowalenga waliokusanyika kwa ibada ndani ya chumba cha mazoezi cha Chuo Kikuu cha Marawi, mji uliokuwa na idadi kubwa kabisa ya Waislam, ambao ulizingirwa na wapiganaji mwaka 2017.
Kikundi cha Islamic State kilidai kuhusika na shambulizi la bomu, ambalo Rais Ferdinand Marcos aliwalaumu magaidi wa kigeni kuhusika.
Polisi walisema huko nyuma walikuwa wakiwafuatilia watu wanne kuhusiana na shambulizi hilo, ambapo jeshi limeeleza kuwa kuna uwezekano lilikuwa ni shambulizi la kulipiza kisasi kwa operesheni zao walizofanya dhidi ya vikundi vya wapiganaji katika mkoa huo.
Washukiwa hao wawili waliotajwa Jumatano – Kadapi Mimbesa na Arsani Membisa – ni wanachama wa kikundi cha Dawlah Islamiyah-Maute, mkurugenzi wa polisi wa mkoa Brigedia Jenerali Allan Nobleza ameuambia mkutano wa waandishi wa habari.
Mtu wa tatu, ambaye hakutambulika, alikuwa anawalinda i mashambulizi, Nobleza alisema.
Manila ilisaini mkataba wa amani na kikundi kikubwa kabisa cha waasi nchini humo, Moro Islamic Liberation Front, mwaka 2014, na kumaliza vita vya uasi vya umwagaji damu.
Lakini bado vipo vikundi vidogo vidogo vya wapiganaji wa Kiislam waliopinga makubaliano hayo ya amani, ikiwemo wapiganaji ambao wanaungana na kikundi cha Islamic State. Waasi wa Kikomunisti pia wanafanya harakati zao katika eneo hilo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP