Hatua hii imechukuliwa baada ya kuzuka kwa mapigano ambayo yamepelekea raia wengi wa kigeni na wa Sudan kukimbia wakihofia usalama wao.
Meli ya kivita ya Ufaransa iliyobeba mamia ya watu walioondolewa ilitia nanga Jumatano asubuhi huko Jeddah , Saudi Arabia.
Hii ni sehemu ya juhudi pana zinazohusisha meli kadhaa za kivita pamoja na usafiri wa ndege.
Ufaransa imetoa mchango mkubwa kupata njia ya kuwaondoa watu wengi kutoka kambi ya jeshi la anga nje ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Msemaji wa jeshi kanali Pierre Gaudilliare alisema Ufaransa iliwaokoa zaidi ya raia 500 kutoka mataifa 40 kwa kutumia ndege mwishoni mwa wiki baada ya kupata kituo cha anga kaskazini mwa Khartoum Jumamosi.